• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Lionel Messi atoa mchango wa pound laki 5 kusaidia katika vita dhidi COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-05-14 16:51:29

    Staa wa Barcelona Lionel Messi kwa mara nyingine tena ameonyesha ukarimu wake baada ya kutoa mchango wa pound laki 5 kusaidia katika vita dhidi ya virusi vya corona nchini Argentina. Awali Messi aliahidi kutoa pauni milioni moja kama njia ya kusaidia katika kudhibiti ugonjwa huo huku nusu za pesa hizo zikitolea katika Hospitali ya Kliniki ya Barcelona na zingine katika vituo vya matibabu nchini humo. Wakati huo huo, wachezaji wa Barcelona wameruhusiwa kurejea mazoezini baada ya kufanyiwa vipimo vya virusi vya corona na matokeo kuonyesha hawana virusi hivyo siku ya Alhamisi, Mei 8. Catalans walikuwa wanatumikia marufuku ya kutotoka nje tangu Machi kwa sababu ya virusi hivyo ambavyo vimewaua wengi Uhispania na mataifa mengine ulimwenguni. Kulingana na ripoti ya Goal, hakuna mchezaji yeyote wa Barcelona ambaye alipatwa na virusi hivyo huku Mfaransa Ousmane Dembele akikosa kupimwa kwa sababu winga huyo wa zamani wa Borussia Dortmund anauguza jereha na atafanyiwa vipimo hivyo wiki ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako