• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KASHFA: Mwendwa awekwa kikaangoni kujibu kuhusu mamilioni AFCON 2019

    (GMT+08:00) 2020-05-22 08:39:04

    Rais wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF), Nick Mwendwa alishinda katika makao makuu ya Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) Alhamisi ya Mei 21, 2020, akihojiwa kuhusiana na madai ya matumizi mabaya ya fedha. Akiwa ameandamana na naibu wake Doris Petra na Afisa Mkuu Mtendaji wa FKF, Barry Otieno, Mwenda alihojiwa kuhusu namna FKF ilivyotumia Sh milioni 244 ambazo zilitolewa na serikali mwaka uliopita kwa ajili ya kuiandaa timu ya taifa ya Harambee Stars kwa fainali za Kombe la Afrika (AFCON) zilizofanyika nchini Misri. Matokeo ya uchungizi wa DCI yatawasilishwa baadaye kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma atakayetathmini iwapo Mwendwa na FKF wana kesi ya kujibu au la. Mwishoni mwa mwaka jana, gazeti la Nation Sport lilifichua jinsi ambavyo Mwendwa, Petra, aliyekuwa Katibu Mkuu wa FKF Robert Muthomi na baadhi ya maafisa wa Kamati Kuu ya FKF walivyojipa marupurupu ya hadi Sh50,000 kwa siku wakati wa kampeni za AFCON nchini Misri. Kuhojiwa kwa Mwendwa kunafanyika siku chache baada ya nahodha wa Stars, Victor Wanyama kuthibitisha kwamba wanasoka wa timu ya taifa ya Kenya bado hawajapata bonasi walizoahidiwa kwa ushindi wa 3-2 waliousajili dhidi ya Tanzania katika mechi ya awamu ya makundi AFCON 2019.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako