Mkutano wa tatu a Awamu ya 13 ya Bunge la Umma la China umefunguliwa leo mjini Beijing. Rais Xi Jinping na viongozi wengine wa Chama cha Kikomunisti cha China na wa serikali, pamoja na wajumbe 2,897 wa Bunge la Umma la China walishiriki.
Kutokana na janga la COVID-19, hii ni mara ya kwanza kwa mkutano huo kuahirishwa hadi mwezi Mei katika miaka 22 iliyopita. Kwenye ufunguzi wa mkutano huo, washiriki wote walikaa kimya kuomboleza vifo vya waliofariki kwenye janga hili.
Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang alitoa ripoti za kazi ya serikali katika mwaka uliopita, kutoa mapendekezo ya kazi za mwaka huu, na kuziwasilisha kujadiliwa kwenye mkutano.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |