Ripoti ya kazi ya serikali iliyoitolewa na serikali ya China imesema, mwaka huu serikali ya China itatekeleza miradi muhimu ya kuhifadhi mfumo wa mazingira ya asili na kuhimiza ujenzi wa ustaarabu wa mazingira ya asili.
Ripoti hiyo inasema inatakiwa kuimarisha viwanda vya kubana matumizi ya nishati na kulinda mazingira kwa kufuata sheria na njia za kisayansi, kupiga marufuku ujangili na biashara ya wanyama pori, pia kuhimiza matumizi ya makaa ya mawe yasiyosababisha uchafuzi wa mazingira, na kuendeleza nishati endelevu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |