Ripoti ya kazi ya serikali ya China imesisitiza kuwa serikali kuu ya China itatekeleza kwa pande zote sera za "Nchi Moja, Mifumo Miwili", "Watu wa Hong Kong kuitawala Hong Kong" na "Watu wa Macau kuitawala Macau", huku ikikamilisha mfumo wa sheria wa kulinda usalama wa taifa wa mikoa yenye utawala maalumu na utaratibu wa utekelezaji. Serikali hiyo itaunga mkono maendeleo ya uchumi wa Hong Kong na Macau, kuboresha maisha ya umma, kuunganisha maendeleo ya maeneo hayo katika mpango wa jumla wa maendeleo ya taifa, ili kudumisha ustawi na utulivu wa Hong Kong.
Ripoti hiyo pia imesisitiza tena sera ya China bara kwa Taiwan, huku ikisisitiza kuimarisha mipango na hatua za ushirikiano kati ya pande mbili za mlango bahari wa Taiwan, kuimarisha maendeleo ya pamoja na kuhakikisha maslahi ya jamaa wa Taiwan, kushikamana na jamaa wote wa Taiwan kupambana na kitendo cha kujaribu kuifanya Taiwan ijitenge kutoka China, kuhimiza umoja na kufungua siku nzuri za baadaye za taifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |