Serikali ya China itaweka kipaumbele katika kuleta utulivu wa soko la ajira na kulinda maisha ya watu, kushinda vita dhidi ya umasikini kwa dhati na kujitahidi kufikia lengo la kukamilisha kazi ya ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote mwaka huu.
Ripoti ya kazi ya serikali iliyowasilishwa leo kwenye mkutano wa mwaka wa bunge la umma la China imeweka lengo la nafasi mpya za ajira mijini nchini China mwaka huu kuwa zaidi ya milioni 9, na kiwango cha ukosefu wa ajira mijini kuwa karibu asilimia sita.
Kutokana na hali ya isiyokadiriwa ya maambukizi ya COVID-19 na hali ya kiuchumi na kibiashara duniani, maendeleo ya China yanakabiliwa na sintofahamu kadhaa. Serikali ya China haijaweka malengo maalum ya ukuaji wa uchumi kwa mwaka huu. Ripoti hiyo pia imesisitiza kwamba China itaendelea na hatua ya kuzuia na kudhibiti virusi vya Corona katika kipindi kijacho, na kushughulikia vizuri maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |