• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika yapaswa kuiga uzoefu wa China katika kuondoa umaskini na kukabiliana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-05-26 09:25:42

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi hivi karibuni alisema, China na Afrika ni ndugu wakubwa wanaopumua kwa pamoja na wenye hatma ya pamoja. Kauli hiyo imefuatiliwa na nchi za Afrika. Katibu mkuu wa chama tawala cha Kenya Jubilee Bw. Raphael Tuju alipohojiwa na mwandishi wa habari wa Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG amesema, China imepata mafanikio makubwa katika kutokomeza umaskini na kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona, na uzoefu wake unastahili kuigwa na nchi za Afrika.

    Kwenye mikutano ya mwaka huu ya Bunge la Umma la China na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, suala la umakini linafuatiliwa zaidi na pande mbalimbali. Ripoti ya kazi za serikali inasema, mwaka huu China itashinda vita dhidi ya umaskini kwa nia thabiti, na kujitahidi kutimiza lengo la ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote. Bw. Tuju amesema mafanikio ya China katika kupunguza umaskini ni mwujiza, na hakuna nchi nyingine inayoweza kuwaondoa watu wengi namna hiyo kutoka kwenye lindi la umaskini kama China ilivyofanya. Anaona mafanikio ya China yameipatia Afrika uzoefu na mwamko katika kukabiliana na umaskini. Anasema,

    "Naona kuwa Kenya inaweza kujifunza vitu vingi kutoka kwa China. Kwanza, tukiwa na mpango na mkakati sahihi, pia tunaweza kufanikiwa. Tumetiwa moyo na uzoefu wa China. Tukijaribu, huenda pia tutafanikiwa. Pili, tunapaswa kujifunza sera zinazotekelezwa na China katika usimamizi wa mambo ya kitaifa, kupambana na ufujaji na ufisadi, ambazo zinaweza kutuwezesha tupate mafanikio kama China."

    Bw. Wang Yi kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kikao cha mkutano wa Bunge la Umma amesema, China na Afrika zitaendelea na ushirikiano katika kukabiliana na janga la virusi vya Corona, zaidi ya viongozi 50 wa nchi za Afrika walitoa salamu za pole na misaada halisi kwa China wakati ilipokabiliwa na mlipuko wa virusi hivyo, na China imetuma vikundi vya madaktari kwa nchi kadhaa za Afrika. Bw. Tuju amesema, mchakato wa kukabiliana na COVID-19 umeonesha umuhimu wa kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, ingawa hali ya maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika si mbaya kama mabara mengine, lakini uzoefu wa China katika kupambana na virusi hivyo unastahili kuigwa na nchi za Afrika. Anasema,

    "Tuna dunia moja tu, ambayo ni makazi ya binadamu wote. Hivyo naona pendekezo la rais Xi Jinping la kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja ni la busara. China ina teknolojia za juu za kisayansi, na uwezo mkubwa wa kuzalisha vifaa tiba, uwezo ambao nchi za Afrika hazina. Hivyo tunanufaika sana katika ushirikiano wetu na China."

    Kutokana na sintofahamu mbalimbali, ripoti ya kazi za serikali ya China haikutaja lengo la ukuaji wa uchumi kwa mwaka huu. Lakini Bw. Tuju ana imani kubwa kuhusu maendeleo ya uchumi wa China. Anasema,

    "Watu wa China wana nia imara, na wanaweza kukabiliana na changamoto yoyote. Naamini kuwa chini ya uongozi thabiti wa rais Xi na Chama cha Kikomunisti cha China, nchi hiyo itashinda matatizo yote, na kupata ustawi zaidi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako