Kocha mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ameripotiwa kuwa kwenye juhudi za kina ili kuhakikisha anarefusha mkataba wa straika Odion Ighalo amalizie mechi za Ligi Kuu England zilizobakia. Lakini wakati hilo linajiri, inadaiwa kwamba klabu ya Shanghai Shenhua ambayo ndiyo inammiliki mchezaji huyo, inamhitaji arudi nchini China ili kwenda kujiunga na timu hiyo ambayo inatarajia kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu nchini wiki chache zijazo. Shenhua inaonekana kutoafiki kitendo cha United kuhitaji kurefusha mkataba wa mkopo wa Ighalo, na badala yake wanataka ikiwa United inahitaji kumbakiza mchezaji huyo imnunue moja kwa moja. Ighalo na wawakilishi wake kwa sasa wanatakiwa kurudi China haraka iwezekanavyo, ingawa mipaka yote ya kuingia nchini imefungwa, lakini itabidi warudi kuja kuweka mambo sawa katika timu yake ili kumaliza mvutano uliopo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |