• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SIMANZI: Nyota wa Liverpool wapiga magoti uwanjani kabla ya mazoezi kufuatia kifo cha George Floyd

    (GMT+08:00) 2020-06-02 08:33:53

    Kikosi cha Liverpool jana Jumatatu kilipiga magoti kwa kuonyesha ishara ya umoja juu ya kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi kabla ya kuanza mazoezi yake katika uwanja wa Anfield. Wachezaji hao kila mmoja alikunja goti moja na kutengeneza duara katikati ya uwanja na kuitazama kamera iliyokuwa ikiwamulika uwanjani hapo. Nyota hao wameonekana kuvalia jezi zenye rangi tofauti tofauti, wengine wakiwa na rangi nyeusi, nyeupe, nyekundu wakati wengine wakiwa wamevalia jezi za mazoezi. Hayo ni mazoezi ya kwanza kwa kikosi cha kocha Jurgen Klopp katika dimba la Anfield tangu kusimama kwa michezo kufuatia kusambaa kwa virusi vya corona.

    Naye mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford amezungumza kufuatia kifo cha Mmarekani mweusi, George Floyd na kusisitiza kuwa watu wana maumivu na wanahitaji majibu, huku maandamano yanazidi kushika kasi ulimwenguni kote. Wanaharakati wamekuwa wakihitaji haki itendeke dhidi ya mauaji ya George Floyd, Mmarekani mweusi ambaye alihujumiwa na polisi mzungu, Derek Chauvin aliyemkandamiza shingoni kwa kutumia goti akiwa amefungwa pingu mjini Minneapolis na kupelekea kifo chake Jumatatu iliyopita. Marcus Rashford amesema kwa muda amekuwa akiwataka watu kuwa wamoja, kufanya kazi pamoja na kuwa kitu kimoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako