• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika CDC yafuatilia kwa karibu mlipuko mpya wa Ebola nchini DRC

    (GMT+08:00) 2020-06-03 20:08:40

    Umoja wa Afrika umesema, Kituo cha Kudhibiti na Kukinga Magonjwa Afrika CDC kinafuatilia kwa karibu hali inavyoendelea huku kikijiandaa kuunga mkono hatua za kukabiliana na mlipuko mpya wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

    Kufuatia ripoti iliyotolewa na mamlaka ya afya katika mkoa wa kaskazini magharibi wa Equateur kuhusu vifo vilivyotokea tarehe 23 na 30 mwezi Mei, serikali ya DRC ilitangaza jumapili kutokea kwa mlipuko mpya wa Ebola katika eneo la Mbandaka, katika mkoa huo.

    Taarifa iliyotolewa na Afrika CDC imesema, huu ni mlipuko wa 11 wa Ebola nchini DRC, na tayari umesababisha vifo vya watu wanne na wengine wanne wameambukizwa katika eneo hilo. Mlipuko huo umetokea wakati wataalam wakijiandaa kutangaza kumalizika kwa mlipuko wa 10 wa Ebola katika mkoa wa Kivu Kaskazini, na wakati nchi hiyo ikijitahidi kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako