• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika yaunga mkono uamuzi wa China kuhusu Hong Kong

    (GMT+08:00) 2020-06-04 17:23:47

    Mkutano wa tatu wa Bunge la 13 la Umma la China hivi karibuni umepitisha Muswada wa Kujenga na Kukamilisha Mfumo wa Sheria wa Kulinda Usalama wa Taifa Katika Mkoa wenye Utawala Maalumu wa Hong Kong na Utekelezaji wa Mfumo huo. Nchi za Afrika zimeunga mkono hatua hiyo, zikisema ni hatua imara iliyopigiwa na China katika kutunga sheria ya usalama wa taifa mkoani Hong Kong, na itatoa uhakikisho kwa ustawi na utulivu wa muda mrefu wa mkoa huo.

    Serikali ya Tanzania imesema inafuatilia kwa karibu suala la Hong Kong, na msimamo wake kuhusu suala hilo ni kama zamani, yaani kuunga mkono sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili". Nchi hiyo inaona kuwa, utekelezaji wa sheria ya usalama wa taifa si kama tu utamaliza ukosefu wa sheria hiyo katika mkoa wa Hong Kong, bali pia utasaidia sehemu hiyo kurejesha utaratibu wa kawaida.

    Katibu mkuu wa Chama tawala cha Kenya Jubilee Raphael Tuju amesema, Hong Kong ni sehemu ya China, na kuingilia kati suala la sehemu hiyo ni kama kuingilia kati mambo ya ndani ya China, kitendo ambacho kinakiuka Makubaliano ya Kimataifa ya Vienna.

    Serikali ya Burundi imetoa taarifa kuhusu sheria hiyo ya China, ikisema inaunga mkono Bunge la Umma la China kupitisha uamuzi kuhusu sheria hiyo, ambayo itakuwa na ufanisi wa kulinda usalama wa taifa katika sehemu ya Hong Kong. Taarifa hiyo pia imesisitiza kuwa Burundi inapinga nguvu yoyote ya nje kuingilia kati mambo ya ndani ya China.

    Serikali ya Uganda imesema Hong Kong ni sehemu isiyotengeka ya China, na suala la sehemu hiyo ni mambo ya ndani ya China. Uganda inafuata sera ya kuwepo kwa China moja duniani, na kuunga mkono kwa nguvu zote China kuzuia ufarakanishaji, na kulinda ustawi na utulivu wa Hong Kong, na kwamba hila ya nchi za Magharibi ya kufarakanisha China haitafanikiwa.

    Msomi maarufu nchini Nigeria Arad Fowler kwenye Gazeti la The Nation la nchi hiyo ametoa makala akifichua unafiki wa nchi za Magharibi, na kusema usalama wa taifa ni suala kuu zaidi, na sheria ya usalama wa taifa iliyopitishwa na Bunge la Umma la China itaokoa Hong Kong.

    Spika wa bunge la Mali Moussa Timbiné amesema, suala la Hongkong ni mambo ya ndani ya China, na nchi nyingine hazina haki ya kuingilia kati suala hilo. Amesisitiza kuwa Mali inaunga mkono kithabiti China kulinda mamalaka na ukamilifu wa ardhi zake, na kutekeleza sera ya "Nchi moja, Mifumo miwili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako