Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool na Manchester City, Mario Balotelli anaripotiwa kufurushwa na klabu ya Italia, Brescia baada ya kutofautiana vikali na rais wa klabu hiyo Massimo Cellino. Balotelli alikuwa amesalia na miaka miwili katika mkataba wake na Brescia kabla ya kupigwa kalamu. Kumekuwa na ripoti za awali kwamba klabu hiyo ilikuwa inapania kumtimua Balotelli baada ya msimu wa 2019/20 kabla ya tukio ya sasa. Kulingana na Football Italia, viongozi wa Brescia walikerwa na hatua ya mshambuliaji huyo kukosa mazoezi kwa siku 10. Ripoti hiyo pia iliongezea kwamba hakuna hatua yoyote ya kisheria itachukuliwa kwa sababu klabu hicho kilimfahamisha wakili wake kabla ya uamuzi huo kufanywa. Baada ya kuchezea Nice na Marseille nchini Ufaransa, Balotelli aliamua kurejea katika taifa lake kuendeleza taaluma yake ya soka mnamo Agosti 2019.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |