• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe asifu ushirikiano kati ya nchi hiyo na China katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-12 16:57:23

    Hafla ya kukabidhi awamu ya pili ya msaada wa vifaa vya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona uliotolewa na serikali ya China kwa Zimbabwe imefanyika Ikulu mjini Harare. Akihutubia katika hafla hiyo, Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema msaada wa China utachangia katika kuhimiza kazi ya kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi nchini Zimbabwe.

    Balozi wa China nchini Zimbabwe Bw. Guo Shaochun alikabidhi vifaa hivyo ikiwemo barakoa za matibabu na vifaa vya kujilinda vya watu binafsi vilivyotolewa na China. Akipokea vifaa hivyo, Rais Mmangagwa ameishukuru serikali na watu wa China kwa kuiunga mkono Zimbabwe. Anasema:

    "Ili kuisaidia Zimbabwe kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona, tumepokea tena vifaa vya kupambana na virusi hivyo vilivyotolewa na China. Wiki iliyopita, Zimbabwe ilipokea wataalamu 12 wa matibabu wa kupambana na maambukizi kutoka China, ambao walibadilishana ujuzi na uzoefu unaostahili kuthaminiwa wa kupambana na virusi hivyo. Kwa niaba ya serikali na watu wa Zimbabwe, natoa shukurani kwa China kutokana na uungaji mkono kithabiti iliyoutoa kwa Zimbabwe katika muda mrefu uliopita."

    Rais Mnangagwa amesema, hivi sasa Zimbabwe iko katika kipindi muhimu cha kukinga na kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona, kwa kuwa idadi ya watu waliothibitishwa kuwa na virusi hivyo ni wale ambao walisafiri kutoka nje ya nchi. Zimbabwe inakabiliwa na changamoto za kudhibiti hali ya maambukizi na kurejesha uzalishaji, hivyo msaada wa China utaisaidia kuongeza uwezo wa kuzuia na kudhibiti maambukizi, na kuimarisha dhamira ya Zimbabwe katika kushinda mapambano hayo. Anasema:

    "Uungaji mkono wa China umechangia sana kazi ya Zimbabwe katika kupambana na maambukizi ya virusi, kuongeza uwezo wa wahudumu wa afya walio mstari wa mbele, na kuwalinda na maambukizi wakati wanapopambana na virusi hivyo. Ushirikiano kati ya Zimbabwe na China katika kupambana na virusi hivyo pia umeonesha mambo halisi katika uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya pande hizo mbili."

    Balozi wa China nchini Zimbabwe Bw. Guo Shaochun ameeleza kuwa, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika kupambana na maambukizi ya virusi umeonesha urafiki wa jadi kati ya nchi hizo, na kuonesha ahadi thabiti za China katika kujenga Jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika. Anasema:

    "China inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa ikiwemo Zimbabwe, kuhimiza ahadi za China kwa Afrika zinatekelezwa kwa ufanisi. China na Zimbabwe zikifanya juhudi kwa pamoja hakika zitashinda katika mapambano dhidi ya virusi na kupata mustakabali mzuri."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako