Misaada hiyo ambayo imetolewa na shirika la Wateraid ni pamoja na mashine saba za kunawia mikono na sabuni lita 720.
Misaada hiyo imekabidhiwa kwa ajili ya kutumiwa katika kituo cha mabasi Ubungo, kituo kikuu cha mabasi yaendayo haraka Gerezani na Kimara Mwisho kwa ajili ya matumizi ya abiria wanaoingia na kutoka katika vituo hivyo.
Kaimu Meya wa jiji la Dar es Salaam Abdallah Mtinika alisema kituo hicho ni cha kisasa ambacho kitakuwa na mahitaji yote na kwamba serikali ilitoa Sh. bilioni 51 kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wake.
Ameongeza kuwa kituo hicho kina uwezo wa kuingiza mabasi 700, magari madogo 80 na nje kutakuwa na eneo lenye uwezo wa kupaki magari 1,000.
Kuhusu msaada waliopokea, aliwataka watumiaji wa vituo hivyo kuzingatia kunawa mikono, ili kujikinga na maambukizo ya virusi vya corona na magonjwa mengine ya kuambukiza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |