Mashindano ya Chess kupitia mtandao wa internet yalioandaliwa na klabu za Don Bosco na Rising Star za jijini Dar es Salaam, Tanzania, yameingia katika awamu ya pili weekend iliyopita. Mashindano hayo yanayojulikana kama Grand Prix Arenas, yanaandaliwa ili kuboresha kiwango cha mchezo huo nchini Tanzania. Awamu ya 12 ya mashindano hayo ilifanyika weekend iliyopita na ilikuwa ya kwanza, ikishirikisha zaidi ya wachezaji 40 kutoka nchi mbalimbali. Mmoja wa waandaaji wa mashindano hayo Kara Louis amesema, Mugema Arthur kutoka Uganda alishinda Don Bosco Arena akiwa na point 25, akifuatiwa na Glenn Golding kutoka Afrika Kusini aliyekuwa na alama 16, na Mtanzania Christian Fernandez alichukua nafasi ya tatu na alama 14.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |