Wakati maudhui ya mkutano wa Focac mwaka huu ikiwa ni vita dhidi ya Covid 19 waafrika wengi wakiwemo viongozi wameendelea kupongeza serikali ya China kutokana na mchango wake mkubwa katika kuzisaidia nchi za Afrika kupambana na virusi hivyo. Baadhi ya misaada ya ambayoi China imetuma katika nchi za Afrika ni pamoja na barakoa, dawa,sanitizers miongoni mwa zingine ambazo zimekuwa zikitumiwa kupiga vita virusi hivyo. Wizara ya mambo ya nje ya Kenya imekuwa mstari wa mbele katika kupongeza China hasa kwa kuhakikisha kuwa hakuna Mkenya hata mmoja ambaye alipoteza maisha yake nchini China kutokana na ugonjwa huo. Waziri msaidizi wa wizara ya mambo ya nje ya Kenya Bw Kamau Macharia anasema hii ni kutokana na juhudi za haraka ambazo China ilichukua kuhakikisha kuwa inaokoa maisha ya binadamu.
"Kama mjuavyo tunakaribu wakenya 3000 nchini China na hata kuna uwezekano wakawa wengi zaidi kwa kuwa kuna wengine ambao hawajajiandikisha ubalozini.Lakini kinachotufurahisha zaidi hakuna kisa cha mkenya ambaye amepoteza maisha yake kutokana na virusi vya Corona nchini China. Hii ni habari njema kwetu kama wakenya.Utakumbuka kuwa wanafunzi wengi wa Kenya walikuwa wakisomea Wuhan lakini serikali ya China ilihakikisha kila mwanafunzi yuko salama na hivi sasa baada ya kufunguliwa kwa mji huo wameanza kutembea bila matatizo yoyote".
Jana pekee idadi ya maambukizo nchini Kenya ilikuwa 184 huku waliopona wakiwa 27 ikiwa ni idadi kubwa ya watu waliotibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Baadhi ya madaktari tulioongea nao wanaona haya ni mafanikio makubwa na wanatarajia mafanikio mengi zaidi baada ya mkutano wa Focac kutokana na ushirikiano kati ya China na Afrika.Akitoa taarifa mpya kuhusu maambukizo ya virusi vya Corona waziri msaidizi Rashid Amana anasema kilivhomvutia zaidi ni kuwa idadi ya watu wanaopona inazidi kuongezeka nah ii ni kutokana na ushirikiano mkubwa ambao wamepata kutoka kwa washirika wa Kenya ikiwemo China.
"Tunafuraha kutangaza kuwa leo tumewapeleka nyumbani wagonjwa 27 wa Covid 19 baada ya kupona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya watu ambao wamepona ugoinjwa huo kufikia 1353. Pia ningependa kusema kuwa wagonjwa wawili waliaga dunia na kufikisha idadi ya vifo kutokana na Corona kufikia 107. Nachukua fursa hii kutoa rambi rambi zetu kwa ndugu, familia na marafiki za waathiriwa wakati huu mgumu".
Katika kufanikisha vita dhidi ya Covid 19 nchi za Afrika zimewataka walioko nje hususan nchini China kuheshimu maagizo yanayotolewa na serikali ikiwa ni mojawapo ya njia za kuendeleza ushirikiano katika kupambana na virusi vya Corona. Waziri Macharia kwa upande wake amesisitiza haja ya wakenya wengi walioko China kuheshimu sheria na maagizo yanayotolewa na serikali ya China katika kupambana na virusi vya Corona.
"Jambo la muhimu hivi sasa tungependa kutuma ujumbe kwa marafiki zetu, ndugu zetu na wanafunzi wetu walioko China kuwa waonyeshe nidhamu kwa serikali ya China wakati inapopambana na virusi hivi vya Corona.Hasa wakati wa upimaji wa virusi vya corona na wakati wanapojilinda dhidi ya ugonjwa huo na muhimu zaidi wakati wa kuheshimu sheria na maagizo ya serikali ya China".
Mkutano wa Focac mwaka huu kwa mara ya kwanza unafanyika kwa njia ya video kutokana na janga la Corona ambalo limeendelea kutikisa dunia .Hata hivyo waafrika wengi wana imani kuwa mada ya mwaka huu ambayo ni ushirikiano katika vita dhidi ya Corona utaziwezesha nchi za Afrika kufanikiwa katika kuutokomeza ugonjwa huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |