• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ahadi mpya ya China yaleta tumaini la maisha mapya katika mapambano ya Afrika dhidi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-18 17:16:33

    Ahadi za China zilizotolewa kwenye mkutano maalumu wa kilele wa Mshikamano wa China na Afrika dhidi ya COVID-19 zitasaidia Afrika kupata vifaa vya matibabu katika kupambana na virusi vya Corona na kuanza mapema ujenzi wa makao makuu ya Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) utasaidia kuleta pumzi mpya katika mapambano dhidi ya virusi hivyo. Hayo yamesemwa jijini Nairobi, Kenya na mtaalam wa Ushirikiano wa Kimataifa hasusuan kuhusu uhusiano kati ya China na Afrika Cavince Adhere.

    Adhere amepongeza ahadi ya China ya kutoa vifaa zaidi, kupeleka timu za wataalam, na kuanza mapema ujenzi wa makao makuu wa Africa CDC.

    Wakati wa Mkutano Maalum wa Mshikamano wa China na Afrika dhidi ya COVID-19 uliofanyika kwa njia ya video, rais wa China Xi Jinping alisema China itaanza ujenzi wa makao makuu ya Africa CDC mwaka huu, kabla ya muda uliopangwa, na itaendelea kuzisaidia nchi za Afrika kwa kutoa vifaa, kupeleka timu za wataalam, na kuiwezesha Afrika kununua vifaa vya matibabu kutoka China.

    Adhere amesema, wakati virusi vya Corona vinaendelea kuliathiri bara la Afrika, hitaji la bara hilo kwa bidhaa muhimu kama vile vifaa vya kupima virusi, dawa, mashine za kupumua, barakoa, na mavazi ya kujikinga limeongezeka zaidi. Amesema mkutano huo umekuja muda mwafaka wakati kesi za virusi vya Corona zikiongezeka katika nchi nyingi za Afrika, na kutoa shinikizo kwa mfumo wa afya uliopo sasa, huku uchumi wa nchi hizo ukiathirika kutokana na hatua za kufunga nchi.

    Mtaalam huyo amesema, tangu mlipuko wa virusi vya Corona ulipotokea, China imesimamia kauli zake kwa vitendo halisi kwa kutoa misaada muhimu kwa bara la Afrika. Pia amesema, uamuzi wa China wa kufuta madeni ya nchi husika za Afrika katika mfumo wa mikopo isiyo na riba kwa serikali ambayo ilitakiwa kuanza kulipwa mwishoni mwa mwaka huu ndani ya Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika ulikuwa ni wa kushangaza na unapaswa kusifiwa.

    Amesema hatua hiyo imekuja wakati sahihi kutokana na maombi ya bara hilo na itasaidia kuachilia rasilimali ambazo zitatumika katika kudhibiti mlipuko wa virusi vya Corona. Pia amesema imetoa moyo sana kusikia China ikizitaka nchi wanachama wa Kundi la Nchi 20 (G20) kufikitia kuongeza muda wa kulipa madeni kwa zile nchi zilizoathirika zaidi na virusi hivyo.

    Akizungumza kauli ya rais Xi kwenye mkutano huo kuwa China inaunga mkono juhudi za Afrika za kuendeleza Eneo la Biashara Huria la Afrika, kuongeza nguvu ya maingiliano na kuimarisha mnyororo wa viwanda na ugavi, Adhere amesema anaamini kuwa hatua hiyo itatoa ajira zilizopotea kutokana na janga la Corona, huku wakati huohuo ikiongeza mwingiliano wa nchi za bara hilo.

    Mtaalam huyo amesema, virusi vya Corona vinajenga dunia mpya, ni tishio ambalo linataka umoja katika lengo na juhudi. Pia amesema hakuna nchi iliyo na kinga ya janga hilo, na nchi zilizo hatarini zaidi kama zile zilizoko barani hazipaswi kuachwa nyuma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako