• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanasiasa wa Marekani wanakwepa ushahidi wa mashambulizi ya kigaidi mkoani Xinjiang

    (GMT+08:00) 2020-06-19 18:55:47

    Mtandao wa Kimataifa wa Televisheni wa Shirika Kuu la Utangazaji la China CGTN leo umetoa filamu inayoonesha hali halisi ya Mlima Tianshan: Kumbukumbu ya Mapambano dhidi ya Ugaidi mkoani Xinjiang.

    Filamu hiyo imefichua uhalifu uliofanywa na magaidi mkoani Xinjiang, na kuonesha haja ya China kufanya mapambano dhidi ya ugaidi, na mafanikio yaliyopatikana.

    Takwimu zisizo rasmi zinaonesha kuwa, kuanzia mwaka 1990 hadi 2016, mkoa wa Xinjiang ulishuhudia maelfu ya mashambulizi ya kigaidi, yaliyosababisha vifo na majeruhi ya watu na hasara kubwa ya kijamii. Lakini baadhi ya wanasiasa wa Marekani wanakwepa kuzungumzia ukweli huo, na badala yake kuwaunga mkono magaidi hao na kuwapa misaada halisi. Mswada wa Marekani wa mwaka 2020 wa Sera za Haki za Binadamu za Wauyghur ni ushahidi mpya wa nchi hiyo kuunga mkono magaidi mkoani Xinjiang.

    Wachambuzi wa kimataifa wanaona kuwa suala la Xinjiang sio suala la kabila, dini na haki za binadamu, bali ni suala la ugaidi na ufarakanishaji. Ili kukabiliana na suala hilo, China ilichukua hatua mbalimbali yenye ufanisi, ikiwemo kuanzisha vituo vya mafunzo ya ufundi stadi, ili vijana maskini ambao ni rahidi kuathiriwa na msimamo mkali kupata ajira. Kutokana na hatua hizo, katika miaka mitatu iliyopita, hakuna shambulizi la kigaidi lililotokea mkoani humo, na mwaka huu, kama sehemu nyingine nchini China, mkoa wa Xinjiang utaondokana na umaskini.

    Kwenye filamu hiyo, Mwuyghur mmoja wa Xinjiang alisema, anatumai watoto wake wanaweza kuishi katika mazingira yenye utulivu, usalama na furaha kama yalivyo hivi sasa. Hayo pia ni matumaini ya wakazi wote wa mkoa huo. Wanasiasa wa Marekani wanapaswa kuacha kuunga mkono magaidi, na kutoingilia kati mambo ya ndani ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako