Chama cha Mchezo wa Magongo Tanzania (THA) kimetangaza kuwa mashindano ya Kombe la Nyerere yatafanyika Oktoba mwaka huu mjini Moshi, Kilimanjaro. Mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha timu za mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar. Katibu Mkuu wa Chama hicho Kaushik Doshi amesema, wachezaji wote wanaendelea vema na mazoezi kwa ajili ya kuonyesha ushindani mkali katika mashindano hayo. Pia amesema, maambukizi ya virusi vya Corona yalivuruga ratiba yao, lakini wanaamini kila mchezaji ataongeza juhudi ili kurejea kwenye ubora baada ya kukaa muda mrefu bila ya kushiriki mashindano yoyote.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |