• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nzige wavamia Delhi India

    (GMT+08:00) 2020-06-28 16:59:46

    Nzige wa jangwani wamevamia Delhi, mji mkuu wa India. Idadi kubwa ya wadudu hao waharibifu jana mchana walianza kuingia maeneo ya Gurgaon, Parval na Devarka, mjini Delhi, na kuelekea jimbo la Uttar Pradesh. Wenyeji waliwafukuza nzige kwa kutengeneza kelele kubwa. Serikali ya mji wa Delhi waliitisha mkutano wa dharura jana alasiri kujadili namna ya kukabiliana na tishio la nzige.

    Kwa mujibu wa tabia ya nzige, wadudu hao husafiri mchana na kutulia baada ya giza, wanaweza kusafiri kilomita 150 kwa siku. Katika eneo la kilomita 1 za mraba, inaweza kuwepo nzige milioni 40 hadi 80, na nzige mmjoa anaweza kula mimea yenye uzito unaolingana na nzige mwenye kila siku, ndio maana ni tishio kubwa kwa usalama wa chakula.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako