Rais Xi Jinping wa China amesisitiza umuhimu wa kutegemea mageuzi kukabiliana na mabadiliko ya mazingira na kufungua maeneo mapya, huku akitoa umuhimu wa utafiti wenye matokeo mazuri katika nyanja muhimu.
Rais Xi amesema hayo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye mkutano wa 14 wa Kamati Kuu ya Mageuzi ya Kina uliofanyika jana hapa Beijing na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo waziri mkuu wa China, Li Keqiang.
Akiongoza mkutano huo, rais Xi amesema mafanikio na nafasi ya uongozi katika mageuzi lazima itumike kikamilifu ili nchi iweze kutimiza malengo na majukumu yaliyoainishwa kwenye mpango wa 13 wa miaka mitano wa maendeleo, kushinda vita dhidi ya umasikini, kumaliza ujezi wa jamii yenye ustawi kwa pande zote, na kuanza awamu mpya kuelekea kujenga nchi ya ujamaa wa kisasa.
Mkutano huo pia ulisikiliza ripoti kuhusu maendeleo ya mageuzi katika mfumo wa afya na tiba yaliyopatikana tangu mkutano wa tatu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |