Leo tarehe mosi Julai ni mwaka wa 99 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China CPC ambacho ni chama kikubwa zaidi cha kisiasa duniani. Chama hicho ambacho wanachama wake wameongezeka kutoka zaidi ya 50 hadi zaidi ya milioni 90 kimetawala China kwa miaka 71. Uchumi wa China umechangia zaidi ya asilimia 30 ya ongezeko la uchumi wa dunia kwa miaka mingi mfululizo, na umekuwa injini muhimu ya ukuaji wa uchumi wa dunia.
Rais Xi Jinping ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC alisema, chama hicho kinazingatia zaidi watu, na kuweza kufanya lolote ili kuhakikisha usalama wa maisha na afya ya watu. Mwaka huu, mlipuko wa virusi vya Corona umeleta changamoto kubwa. Dunia imeshuhudia kuwa chama hicho kimeongoza wananchi wa China kujenga "Ukuta Mkuu" dhidi ya virusi hivyo.
Katika vita dhidi ya virusi vya Corona, wanachama wengi wa CPC wakiwemo Zhong Nanshan na Li Lanjuan wamejitolea na kuwa mstari wa mbele zaidi. Takwimu zinaonesha kuwa takriban wanachama milioni 30 wa CPC wameshiriki kwenye mapambano hayo moja kwa moja, na kati yao watu 396 walijitoa mhanga.
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Chama cha Kikomunisti cha Russia Gennady Zyuganov amesema, Wachina wamepata mafanikio makubwa katika vita dhidi ya virusi vya Corona chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China. Aidha, China pia imezisaidia nchi nyingine kukabiliana na virusi hivyo, na kuthibitisha wazo la jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja kwa hatua halisi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |