Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa UNAIDS, inaonyesha kuwa lengo la kutokomeza UKIMWI duniani katika mwaka 2020 halitatimizwa. Mkurugenzi wa shirika hilo Winnie Byanyima amesema, ingawa juhudi za kutokomeza UKIMWI zimepata mafanikio kadhaa, lakini bado kuna upungufu, yaani haziwezi kupanua zaidi mafanikio hayo.
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa ingawa mafanikio ya mapambano dhidi ya UKIMWI ni dhahiri, lakini bado hayana usawa, hasa katika kupanua matibabu ya kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi. Kutokana na nchi mbalimbali duniani haziwezi kunufaika na mafanikio hayo kwa usawa, ukosefu wa kutenga raslimali, na maambukizi ya virusi vya Corona, lengo la mapambano dhidi ya UKIMWI la mwaka huu halitatimizwa.
Bibi Byanyima amesema kwa sasa kuna watu milioni 38 walioambukizwa virusi vya UKIMWI, wengi kati yao ni vijana, na wanaopata matibabu ni milioni 25.4 tu, maana wagonjwa milioni 12.6 bado wanasubiri matibabu. Mwaka jana, idadi ya watu waliokufa kutokana na UKIMWI ilifikia laki 6.9.
Bibi Byanyima amesema baadhi ya nchi zimeonyesha nia ya kisiasa, na kutenga rasilimali kwa ajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI, kwa hivyo idadi ya vifo imepunguzwa. Kwa mfano kiwango cha vifo kutokana na UKIMWI nchini Afrika Kusini kimepungua kwa asilimia 53 katika miaka 10 iliyopita.
Ili kutimiza lengo la kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030, UNAIDS imeweka malengo matatu kutimizwa mwaka 2020, yaani asilimia 90 ya watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI wanajua hali zao, asilimia 90 ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi hivyo wanapata matibabu, na asilimia 90 ya watu wanaopata matibabu hali ya virusi mwilini iwe imedhibitiwa.
Kutokana na theluthi mbili ya watu walioambukizwa UKIMWI wako katika bara la Afrika, Bibi Byanyima amependekeza hatua halisi katika bara la Afrika zikiwemo kupunguza hatari kwa wanawake na wasichana kuambukizwa, kwa mfano kuwafanya wawe shuleni, kuwapatia haki za afya ya kijinsia na afya ya uzazi, na kuwapatia elimu ya jinsia kwa pande zote.
Alipozungumzia maendeleo ya mapambano dhidi ya UKIMWI katika bara la Afrika, Bibi Byanyima amesifu mchango wa China katika kuunga mkono Afrika kujenga uwezo wa afya hasa katika mapambano dhidi ya UKIMWI. Amesema China imeunga mkono nchi za Afrika kuimarisha mfumo wa afya, kujenga kituo cha CDC cha Afrika, pia inazisaidia nchi za Afrika kupambana na magonjwa, hususan UKIMWI na virusi vya Corona.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |