Takwimu zilizotolewa na Kituo cha kukinga na kudhibiti magonjwa cha Afrika zinaonesha kuwa, hadi sasa Afrika ina maambukizi laki 4.9 ya COVID-19, idadi ya vifo ni 11,652 na wagonjwa laki 2.38 wametibiwa.
Ikulu ya Gambia imetoa taarifa kuwa, rais Adama Barrow wa nchi hiyo ametangaza kurefusha hali ya dharura ya nchi hiyo kwa siku 7 zaidi, na hatua zote za udhibiti zinaendelea kufanya kazi.
Shirikisho kuu la biashara la waChina wanaoishi nchini Botswana na kituo cha utoaji wa huduma cha China cha Gaborone wametoa dola za Marekani laki 2.8 kwa ajili ya mfuko wa kupambana na virusi vya Corona wa nchi hiyo. Makamu rais wa nchi hiyo Slumber Tsogwane ameshukuru na kusema Botswana inaendelea kulegeza hatua za udhibiti ili kufufua uchumi, na itaendelea kushirikiana na pande mbalimbali kupambana na virusi hivyo.
Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amemwondoa madarakani waziri wa afya wa nchi hiyo Bw. Obadiah Moyo kutokana na tuhumza za rushwa katika manunuzi ya vifaa vya kupambana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Corona vyenye thamani ya dola za Marekani milioni 60.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |