Kocha wa zamani wa klabu ya Arsenal Unai Emery sasa ametangaza rasmi kurejea kufundisha soka nchini Hispania kama kocha mkuu wa klabu ya Villarreal, baada ya klabu hiyo leo kumtambulisha rasmi kama kocha wao mkuu toka afutwe kazi na Arsenal. Unai Emery, 48, anajiunga na Villarreal kama mrithi wa kocha Javi Calleja aliyeoondoka kwenye timu hiyo licha ya kumaliza msimu akiiacha Villarreal nafasi ya tano katika msimamo wa LaLiga na kupata nafasi ya kucheza Europa League msimu ujao. Hii ni mara ya kwanza Unai anarudi kufundisha timu toka alipofukuzwa na Arsenal mwezi Novemba 2019 baada ya kudumu kwa miezi 18 pekee, akiwa kajiunga nao Mei 2018 kurithi mikoba ya Arsene Wenger, Unai amewahi kufundisha kwa mafanikio vilabu vya PSG, Sevilla na Valencia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |