Shirikisho la Soka la nchini Afrika Kusini (SAFA) limemfutia vibali vya kazi Luc Eymael aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu ya Yanga kufanya kazi ndani ya nchi Afrika Kusini. Baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli kocha huyo alisambaza taarifa ambazo zilikuwa zinaonyesha ubaguzi wa rangi na kusema watanzania hawajui soka, na kutumia lugha kadhaa ambazo zilitafsiriwa kuwa ni ubaguzi wa rangi. Yanga ilishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na David Molinga, lakini malalamiko yake yanaonekana kuchochewa na hasira ya kuzomewa na mashabiki wa Yanga. Tayari Yanga imeshamfuta kazi Eymael jumla kutokana na kitendo hicho na kuomba radhi kwa mashabiki, Serikali na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF). Kocha huyo pia aliomba msamaha kwa kueleza kuwa alifanya hivyo kutokana na hasira alizokuwa nazo kwa kupitia kipindi kigumu ndani ya Yanga.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |