Klabu ya PSG ya Ufaransa imekata tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya UEFA Champions League kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1995. PSG chini ya kocha Thomas Tuchels ilifunga mabao mawili katika dakika za lala salama na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Atalanta BC ya Italia. Atalanta walikuwa wa kwanza kupata bao kipindi cha kwanza dakika ya 27 bao ambalo lilifungwa na Mario Pasalic ambalo lilikuwa ni mbao lake la 12 msimu huu kwenye michuano yote. Mabao mawili ya PSG yalifungwa ndani ya Sekunde 149, Marquinhos aliisawazishia PSG dakika ya 89 na sekunde 35 na Choupo-Moting akafunga bao la ushindi katika dakika ya pili na sekunde 4 ndani ya dakika tatu za nyongeza zilizokuwa zimeongezwa na mwamuzi Anthony Taylor. hivyo PSG walifunga mabao hayo ndani ya sekunde 149. Mara ya mwisho PSG kucheza mchezo wa nusu fainali ya michuano hii ilikuwa msimu wa 1994-95 chini ya kocha Luis Fernandez, ambapo waliminjyana na Ac Milan na walitolewa kwa kufungwa jumla ya mabao 3-0 kwenye mchezo wa mikondo miwili. Katika Hatua ya nusu Fainali PSG watacheza na mshindi wa mchezo mwingine wa robo fainali kati ya RB Leipzing na Atletico Madrid itakaochezwa usiku wa leo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |