• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barcelona yasema Koeman ni kocha wao na Messi ni sehemu muhimu ya mpango wao

    (GMT+08:00) 2020-08-19 16:54:48

    Siku tatu baada ya Barcelona kutangaza kuachana na kocha Quique Setien baada ya kudhalilishwa kwa kichapo cha 8-2 kutoka kwa Bayern Munich kwenye robo-fainali za Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) jijini Lisbon, Ureno, ni rasimu sasa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Ronald Koeman ndiye kocha wa Barcelona. Koeman sio mgeni kwenye klabu hiyo, kwani aliichezea klabu hiyo kwa mafanikio kati ya 1989 na 1995. Setien ambaye pia amewahi kuwa kocha wa Real Betis, aliajiriwa na Barcelona mnamo Januari mwaka huu na alikuwa amesimamia jumla ya mechi 25 za Barcelona hadi kutimuliwa kwake. Chini ya uongozi wake, kwa mara ya kwanza tangu 2013-14 Barcelona wamekamilisha kampeni zao za msimu huu bila taji lolote. Kwenye ligi wamekuwa nafasi ya pili nyuma ya Real Madrid. Mkuu wa Barcelona Josep Batromeu ametangaza na kuthibitisha uamuzi wa kumwajiri Koeman na kusema kuwa Leonel Messi ni sehemu ya mpango wa baadaye wa Barcelona. Wiki hii kumekuwa na habari kuwa Messi anataka kuondoka Barcelona, baada ya mwaka mzima wa sintofahamu, huku akishutumiwa kuwa yeye anajiona ni bora zaidi kuliko kocha na hata kuliko klabu nzima, na kumfanya alazimike kutoa lugha kali katika baadhi ya nyakati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako