Kocha Mkuu wa Yanga, Zlatko Krmpotic amesema tatizo kubwa lililopo kwa wachezaji wake wa Yanga, ni kutokuwa na pumzi ya kutosha kutokana na kuwa na maandalizi ya muda mfupi kwa ajili ya msimu mpya wa 2020/21. Yanga ilianza mchezo wa kwanza dhidi ya Tanzania Prisons, Septemba 6 katika Uwanja wa Mkapa na ililazimisha sare ya kufungana goli moja kwa moja. Prisons ilianza kupachika bao dakika ya 7 kupitia kwa Lambart Charles ambalo lilisawazishwa na nyota mpya wa Yanga, Michael Sarpong dakika ya 19. Zlatko amesema amekitazama kikosi namna kilivyocheza kwa umakini, na kugundua tatizo lilikuwa kwenye pumzi na kuwafanya wapate taabu kupata ushindi. Yanga ina kibarua kingine tena Septemba 13 dhidi ya Mbeya City iliyopoteza kwa kufungwa mabao 4-0 na KMC, mechi itaklayochezwa katika Uwanja wa Mkapa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |