• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kukabiliana na changamoto za kimataifa

    (GMT+08:00) 2020-09-08 18:50:47

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing katika mkutano wa kuwatunukia watu hodari waliotoa mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya COVID-19, amesema China itaendelea kushikilia dhana ya jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, na kushirikiana na jamii ya kimataifa katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili dunia.

    Rais Xi amesema China itaendelea kuhimiza ushirikiano wa kimataifa wa kukinga na kudhibiti janga la COVID-19, kuliunga mkono shirika la afya duniani kuongoza mapambano dhidi ya janga hilo, kuchangia uzoefu wake wa kukinga, kudhibiti na kutibu virusi vya Corona na nchi mbalimbali, na kuhimiza ujenzi wa mustakbali wa pamoja wa afya ya binadamu.

    Rais Xi pia amesema China itapanua ushirikiano wa kunufaishana na nchi mbalimbali duniani, kuhimiza mafungamano ya kiuchumi duniani, kulinda mfumo wa biashara wa pande nyingi, kuhakikisha mnyororo wa ugavi duniani unafanya kazi bila matatizo, na kusukuma mbele kwa pamoja ufufuaji na ustawi wa uchumi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako