Wizara ya Afya ya Ethiopia imetangaza kuwa nchi hiyo itaanza kutengeneza vifaa vyake vya kupima virusi vya corona kwa msaada wa China.
Wizara hiyo imesema maandalizi ya ushirikiano na China yanaenda vizuri.
Naibu Waziri wa Afya, Dk Dereje Duguma amesema Waziri Mkuu Abiy Ahmed anashauri serikali ya China kuhusu utengenezaji huo unaotarajiwa kuanza mwezi huu.
Nchi hiyo pia imepanga kuza nje bidhaa za ziada hasa kwa mataifa mengine ya Afrika.
Kwa sasa kuna vituo 52 vya kupima corona nchini Ethiopia na vinapina zaidi ya watu 20,000 kila siku.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |