Benki ya Exim Tanzania imemteua Balozi Juma Mwapachu kuwa mwenyekiti wake mpya wa Bodi ya Wakurugenzi, akichukua nafasi ya Said Mwema.
Mwema amemaliza muda wake kwa mafanikio kulingana na sera ya uongozi wa benki hiyo.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari jana, Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo imemshukuru Balozi Mwapachu kwa uongozi wake wa mfano na mchango wake akiwa kama Mkurugenzi katika Bodi hiyo tangu 2011 ikibainisha kuwa akiwa Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Balozi Mwapachu alihakikisha kuwa benki hiyo inaendelea kusonga mbele kimkakati na kiutendaji.
Balozi Mwapachu ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi, Bodi ya Wakurugenzi, kampuni ya Heritage Insurance Tanzania Limited tangu 1998 ana uzoefu mkubwa akiwa amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, katika mashirika ya umma, sekta binafsi na kwenye asasi za kiraia nchini Tanzania, kikanda na kimataifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |