SERIKALI ya Kenya imewahakikishia wawekezaji katika sekta ya utalii kwamba inaweka juhudi kukabiliana na virusi vya corona ili kuzuia maambukizi kutoka nchi za kigeni baada ya kufunguliwa kwa viwanja vya kimataifa vya ndege.
Mkuu wa idara ya afya ya umma katika Wizara ya Utalii, Bi Susan Mutua, alisema serikali inajizatiti kukabiliana na tishio la maambukizi ya kigeni kutoka kwa wageni wanaoingia humu nchini kupitia viwanja vya kimataifa vya ndege na madereva mipakani.
Mnamo Agosti 1, 2020, serikali ilifungua rasmi viwanja vya kimataifa vya ndege, huku wawekezaji katika sekta ya utalii wakijizatiti kutafuta watalii baada ya soko hilo kudorora kwa sababu ya janga la corona.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |