Wakulima wa pamba katika maeneo ya Kanda ya Ziwa nchini Tanzania watanufaika na mkopo wa zaidi ya Sh. bilioni 11 wa masharti nafuu ambao umetolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini humo (TADB).
Maeneo hayo ni Chato, Biharamulo, Kahama, Msalala, Ushetu na Muleba.
Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Kilimo na Masoko (AMCOS- Chato), Elias Kaswahili, amesema pia TADB imewapa mashine ndogo ndogo za kusindika mazao ya pamba naalizeti.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |