Wizara ya Elimu nchini Kenya itatumia Sh1.9 bilioni kununua madawati maalum kwa wanafunzi wa shule za msingi na upili nchini humo kabla ya shule kufunguliwa hivi karibuni.
Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amesema serikali inalenga kuhakikisha usalama wa wanafunzi kabla ya kufunguliwa kwa shule.
Akiongea wakati wa ziara alizofanya katika chuo kikuu cha Mombasa na kile cha Pwani kilichoko Kilifi, Bw Magoha amesema makamishna wa kaunti 47 nchini watasimamia mfumo wa madawati hayo ili kuhakikisha yanawiana na masharti ya Shirika la Afya Duniani ya watu kutokaribiana.
Profesa Magoha alisema ni sharti shule za chekechea,msingi ,upili na vyuo vikuu vifuate masharti ya WHO dhidi a kujikinga na COVID-19.
Magoha aidha alidokeza kuwa kufuatia agizo la Rais Kenyatta , fedha za madawati tayari zimashatengwa.
Profesa Magoha alisema utengenezaji wa madawati hayo utatoa fursa za ajira kwa mafundi seremala wa ndani kwani madawati hayo yataundwa na sekta ya juakali zilizoko wilayani kabla ufunguzi wa shule.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |