Chama cha Wanawake wenye Viwanda na Biashara nchini Tanzania (TWCC) kimezindua tuzo za wanawake waliofanya vizuri zaidi mwaka 2020 katika sekta za viwanda na biashara nchini humo.
Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Novemba 28, 2020 Jijini Dar es salaam na kuambatana na uzinduzi wa Jarida la Wanawake 100 Wajasiriamali waliothubutu (Tanzania Inspire & Impact Women Book) litakalotumika kutangaza kazi mbalimbali za wanawake wajasiriamali nchini humo.
Mwenyekiti wa TWCC, Jacquiline Maleko alizindua tuzo hizo jana Jijini Dar es salaam, mbele ya waandishi wa habari na kusema zoezi la usajili kwa ajili ya tuzo hizo ni bure na limefunguliwa Septemba 9,2020 na pia zitawahusu wanawake wote wajasiriamali hata ambao sio wanachama wa TWCC.
Aidha Bi.Maleko alisema tuzo hizo zinalenga kuonesha mchango wa mwanamke mjasiriamali katika kukuza uchumi wa nchi na kuchochea maendelo ya jamii.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |