Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limeonya kwamba mlipuko wa nzige uliozuka Kusini mwa afrika unatishia uhakika wa chakula na limetaka hatua zichukulie haraka kuzuia janga kubwa la kibinadamu na kunusuru mamilioni ya watu Botswana, Namibia, Zambia na Zimbabwe.
FAO hivi sasa imezindua mkakati wa hatua za kudhibiti wimbi hilo la nzige ambapo watu takriban milioni 7 katika nchi hizo nne ambao bado wanajikwamua kutokana kwenye ukame wa mwaka 2019 na sasa athari za kiuchumi na kijamii za janga la corona huenda wakakabiliwa hali mbaya zaidi ya kutokuwa na uhakika wa chakula na lishe.
FAO inashirikiana na jumuiya ya maedeleo kwa nchi za Kusini mwa afrika SADC na shirika la kimataifa la kudhibiti nzige wekundu kwa nchi za katikati na Kusini mwa Afrika, kusaidia serikali za nchi zilizoathirika kudhibiti nzige hao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |