Uchumi wa taifa la Afrika Kusini umepungua kwa zaidi ya nusu, katika robo ya mwaka baada ya biashara nyingi nchini humu kulemazwa na makali ya janga la COVID-19. Hii kwa mujibu wa takwimu za kitaifa nchini humo.
Kulingana na takwimu hizo, uchumi ulipungua kwa asilimia 51 kwa robo ya kwanza ya mwaka huu,ikilinganishwa na robo ya mwaka uliopita.
Upungufu huu ulitokana na masharti ya kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona, ulioanza kutekelezwa tarehe 27 mwezi Machi mwaka huu. Sekta zilizoathirika vinaya ni ujenzi, viwanda na uchimbaji madini. Shughuli katika sekta hizi zilipungua hadi asilimia 70.
Uchumiwa taifa la Afrika Kusini ulipungua kwa asilimia mbili kwa mieiz mitatu ya kwanza ya mwaka huu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |