• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kebs Yaharibu Kwa Kuteketeza Bidhaa Ambazo Muda Wa Matumizi Ulipita

    (GMT+08:00) 2020-09-14 16:51:46

    Shirika la Kukadiria Ubora wa Bidhaa Nchini Kenya (Kebs) limeteketeza tani 64 za mchele na spaghetti, bidhaa hizi zikiwa za thamani ya Sh10 milioni mjini Mombasa katika juhudi zake za kuendelea kudhibiti matumizi ya bidhaa ghushi na zilizoharibika nchini.

    Kulingana na mkuu wa shirika hilo katika eneo la Pwani Bw Cirus Wambani shehena hiyo haikuwa salama kwa matumizi ya binadamu.

    Alisema japo shehena hiyo iliingizwa nchini kihalali ilichukuwa muda mwingi katika maghala hadi kuharibika.

    Akizungumza wakati shughuli ya uteketezaji ikiendelea katika eneo la Kibarani Bw Wambani alisema shehena hiyo ilikuwa tani 58 za spaghetti za Ziana na mchele tani sita zilizokuwa zimewekwa katika maghala mbalimbali eneo la Shimanzi.

    Mkuu huyo alisema wamekaza kamba katika kusaka bidhaa ambazo hazifai kuliwa na binadamu. Kilingana na afisa wa uchunguzi wa makosa ya jinai mjini Mombasa (CID) Bw Washington Njiru shehena hiyo iliingia nchini mwaka 2017 na muda wa kuharibika ulikuwa Julai 2019.

    Alisema walinasa shehena hiyo ambayo waliamini kuwa ingepakiwa upya na kusambazwa sokoni kwa ushirikiano wa mafisadi mbalimbali katika serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako