Serikali imesema licha ya utekelezaji wa sera ya uwekezaji ya mwaka wa 1996 kusaidia nchi kuingia kwenye uchumi wa kati, bado kuna vikwazo vine vinavyoikabili sekta hiyo. Baadhi ya vikwazo hivyo ni kikodi na visivyo vya kikodi.
Akizungumza mwishoni mwa wiki jana wakati wa ufunguzi wa warsha ya kutathmini sera hiyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dorothy Mwaluko, alisema vikwazo vingine ni utaratibu wa masuala ya uwekezaji, utangazaji wa fursa za uwekezaji na uwezeshaji uwekezaji.
Mwaluko alisema serikali ya kitaifa imeendelea kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji ili kuiwezesha sekta binafsi kuwa shindani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |