Hata hivyo, Msemaji wa Idara hiyo Bw. Fu Linghui amesema, viashiria vingi viko chini kuliko mwaka jana wakati kama huo, na uendeshaji wa uchumi bado unakabiliwa na changamoto nyingi. Ameongeza kuwa uchumi wa dunia unakabiliwa na changamoto kubwa kufufuka, haswa kutokana na kuwa maambukizi ya virusi vya Corona hayajazuiliwa kwa hatua zenye ufanisi, na sintofahamu ni kubwa. Katika kipindi kijacho China itaendelea kutekeleza vizuri hatua za kuhimiza uchumi kurejeshwa kwa hatua madhubuti.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |