Waendeshaji magari jijini Nairobi kwa mwezi mmoja ujao watalipa zaidi kwa mafuta ya petroli baada ya shirika la udhibiti wa nishati kupandisha bei ya bidhaa hiyo kwa Sh1.48 na kuuza kwa Sh105.43, ikilinganishwa na Sh100.48 ya mwezi uliopita.
Tume imesema kupanda kwa bei ya mafuta ni kutokana na gharama ya uagizaji katika miezi ya hivi karibuni.
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli hata hivyo imepunguza bei ya dizeli na mafuta ya taa kwa Sh0.12 na 0.50 kwa lita kwa wafanyibiashara kwa Sh94.51 na Sh83.15 mtawaliwa.
Eneo la pwani sasa litauza Super Petroli, Dizeli na mafuta ya taa sasa ni Sh103.05, Sh92.15, na Sh80.78 mtawaliwa.
Mjini Kisumu, bei mpya za Super Petroli, Dizeli na mafuta ya taa sasa ni Sh106.06, Sh95.35 na Sh84.02.
Waendeshaji magari huko Nakuru watanunua petroli kwa Sh105.15, Sh94.45 kwa dizeli na Sh83.11 kwa mafuta ya taa kwa lita.
Huko Eldoret, waendeshaji magari watanunua mafuta ya petrol kwa Sh106.07, Sh95.36 kwa dizeli na Sh84.02 kwa mafuta ya taa.
Bei mpya zitaanza kutumika leo hadi Oktoba 14 2020.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |