Shirika la Nishati la Kimataifa (IEA) limepunguza utabiri wa mahitaji ya mafuta ya 2020, likitoa tahadhari kuhusua kasi ya kufufuka kwa uchumi kutokana na janga la corona.
Shirika hilo lenye makao yake makuu mjini Paris Ufaransa limepunguza matarajio yake ya 2020 kwa mapipa 200,000 kwa siku (bpd) hadi mapipa milioni 91.7.
IEA imesema, kuongezeka upya kwa maambukizi ya COVID-19 katika nchi nyingi na hatua za ufungaji, kuendelea kufanyia nyumbani na kupungua kwa oparesheni za uchukuzi wa anga zimechangia kupungua kwa mahitaji ya mafuta.
Limesema China ambayo ilikuwa ya kwanza kufungua kuliko nchi nyingine zenye uchumi mkubwa duniani ilisaidia kuongeza mahitaji ya mafuta, lakini kuongezeka kwa virusi nchini India kulichangia kupungua kwa mahitaji makubwa tangu Aprili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |