Nahodha na mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi anaongoza kwenye orodha ya wanasoka wanapata fedha kubwa duniani, kwa mujibu wa Jarida la Forbes. Malipo ya mshambuliaji huyo raia wa Argentina, yanamfanya kuwa mwanasoka anayelipwa fedha nyingi kuliko wachezaji wengine, akimuacha kwa mbali mpinzani wake wa karibu, Cristiano Ronaldo, anayeshika nafasi ya pili kwenye orodha hiyo. Uchunguzi uliofanywa na Forbes umebaini, Messi anakusanya kiasi cha dola za Marekani milioni 126 kwa mwaka huku Ronaldo akiingiza dola milioni 117. Washambuliaji wa mabingwa wa Ufaransa PSG, Neymar na Kylian Mbappe wanafuatia katika nafasi ya tatu na ya nne.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |