Wanawake nchini Kenya wanashikilia nafasi nyingi za uongozi katika sekta ya viwanda kuliko wanaume.
Haya ni kwa mujibu utafiti mpya wa Chama cha Watengezaji Bidhaa Kenya (KAM).
Ripoti hiyo ya kwanza ya "Wanawake katika sekta ya utengenezaji bidhaa" inaonyesha kuwa wanaume wanamiliki mgao mkubwa wa wafanyakazi wote (64%) kilinganishwa na asilimia 36 ya uwakilishi wa wanawake.
Kulingana na uanachama wa KAM ,makampuni katika sekta ya utengenezaji bidhaa kwa kiwango kikubwa yanamilikiwa na wanaume,hata hivyo kwa ujumla wanawake wanawake wanashikilia nafasi nyingi za uongozi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |