Hivi sasa,wazazi wanalazimika kwenda umbali mrefu kufikia maduka ya vitabu ili kuchagua vitabu kwa ajili ya watoto wao,na mara nyingi baadhi ya vitabu haviwekwi katika rafu kwa sababu ya ukosefu wa nafasi.
Hali hii inaonekana kubadilika huku kampuni ya Longhorn Publishgers Uganda ikisaini mkataba na soko la mtandaoni linalokua kwa kasi nchini Uganda la Suubula.com,ili kuuza vitabu mtandaoni.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Suubula.com,Camble Hope amesema kinachohitajika ni mtu kuingia kwenye mtandao wa Suubula.com na kutafuta vitabu vya Longhorn.Alisema hapo mtu atapata mamia ya vitabu vya elimu vyenye ubora vya kuwasaidia na kuwaongoza watoto katika elimu yao yote.
Aliongeza kuwa baada ya hapo unafanya malipo kama ulivyoongozwa katika mtandao wa Suubula.com halafu vitabu hivyo vitawasilishwa nyumbani au kazini kwako ndani ya kipindi cha masaa 24.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |