Kampuni ya madalali ya Sannex nchini Kenya imetangaza kuwa jumanne wiki ijayo,tarehe 22 Septemba,watauza kwa mnada bidhaa za kampuni ya maduka makubwa ya Tuskys mtaani Donholm baada ya tawi la Greenspan la duka hilo kushindwa kulipa kodi ya nyumba ya karibu Ksh30.8 milioni.
Mwezi uliopita,kampuni ya kudhibiti hasara na usimamizi wa hatari ya Syndicate Agencies Ltd iliwasilisha kesi mahakamani ikidai kuwa kampuni ya maduka makubwa ya rejareja ya Tuskys imeshindwa kulipa deni la la Ksh30.8 milioni ambalo limekusanyika kwa zaidi ya miaka mitatu.
Kampuni hiyo,katika nyaraka za mahakama,zilizowasilishwa tarehe 12 Agosti,inasema kuwa imefanya uchunguzi wa kina na kubaini kuwa hakuna pesa katika akaunti zote za benki za Tuskys na kwamba hakuna taasisi yoyote ya kifedha inayoweka pesa kwa niaba ya Tuskys.Kampuni hiyo ya Syndicate Agencies Ltd ilialika wadeni wengine kujumuika nao katika kesi hiyo.
Masaibu ya Kampuni ya Tuskys hayakuishia hapo,jumatatu tarehe 14 Septemba,kampuni ya madalali ya Sannex Auctioneers ilizuia kampuni ya Tuskys kufungua milango ya duka lake tawi la Greenspan kwa sababu mwenye jumba anawadai wapangaji wake ambao ni duka la Tuskys Ksh30 milioni katika malimbikizi ya kodi ambayo hawajalipa kwa muda mrefu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |