• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Ujenzi wa meli kubwa Ziwa Victoria waanza rasmi

    (GMT+08:00) 2020-09-17 19:53:59

    Ujenzi wa meli kubwa katika Ziwa Victoria umeanza rasmi baada ya kukamilika kwa uwekaji wa Mkuku (Keel Laying) wa meli mpya ya "Mv. Mwanza hapa kazi tu" inayojengwa katika chelezo.

    Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli ( MSCL) Eric Hamiss alieleza kuwa hiyo ndio hatua ya kuanza ujenzi na uunganishaji wa msingi wa meli ili kupata msingi wote wa meli, ambapo kwenye msingi huo utakuwa na kwenye vipande na una kina cha Mita 3.75 ambacho hufikiwa wakati meli imebeba mzigo wote.

    Hamiss alisema kuwa kukamilika kwa msingi huu wa meli kutawezesha ujenzi wa meli kwenda kwa kasi kuliko kasi ya awali.

    Aliongeza kuwa kampuni inayofanya kazi ya ujenzi wa meli hiyo inaitwa GAS Entec, na Kampuni ya KANGNAM Corporation zote kutoka Korea ya Kusini zikishirikiana na SUMA JKT ya Tanzania kwa gharama ya Dola za Kimarekani 39,000,000 sawa na shilling Billion 89.764.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako