Mshambuliaji wa Paris St-Germain, Neymar amepigwa marufuku kucheza mechi mbili baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu dhidi ya Marseille, lakini, mamlaka za soka za Ufaransa zitachunguza madai yake ya ubaguzi wa rangi. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil alikuwa wa mwisho kati ya kadi nyekundu tano katika mechi mbaya ya 'Ligue 1' baada ya kumpiga beki wa Marseille, Alvaro Gonzalez. Neymar baadaye alimshtaki mpinzani wake kwa ubaguzi wa rangi kwenye mitandao ya kijamii na akahimiza mamlaka kutumia 'VAR' kuchunguza. Hata hivyo, Gonzalez amekana madai ya Neymar.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |