• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Museveni aunga mkono mpango wa maendeleo

    (GMT+08:00) 2020-09-18 16:38:58

    Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ameelezea kuunga mkono kwake katika kuongeza ufadhili wa mipango muhimu inayokusudiwa kuinua wanawake na vijana walio katika mazingira magumu ya umaskini.

    Aliyasema hayo katika hafla kukabidhi vifaa vya kisasa vya kuanzisha biashara walivyokabidhiwa vijana na wanawake 3,228 ambao walipangwa katika vikundi 190 katika mkoa mdogo wa Busoga.

    Museveni alisema kuwa Kadaga ana haki ya kutaka pesa zaidi ziingizwe katika programu ambazo zinaondoa umaskini badala ya kupata pesa za kuongeza mishahara ya wafanyakazi wa umma.

    Alisema hapo awali,viongozi wengine walikuwa wakisema wanaweka pesa katika mishahara na vitu vyengine, lakini sasa zinapaswa kuwekwa katika miundombinu na miradi ya kutokomeza umaskini.

    Kadaga alitaja pesa hizo kuwa Shilingi 50 bilioni kwa Programu ya ajira ya Kijani, Shilingi bilioni 30 kwa mpango wa Kujitolea wa Kitaifa wa Wanafunzi na Wahitimu, Shilingi bilioni 30 kwa Mradi wa Uhamasishaji Kijani wa Uganda (UGIP) – Songhai Model, Kazi za Shilingi bilioni 100 kwa Vijana wa Mjini (JOY), Shilingi 20 bilioni kwa Upataji wa haki ya Kazi na Sh50 bilioni kwa kuboresha uzalishaji wa kazi.

    Mpango wa ajira ya Kijani ni mpango mkakati wa Serikali wa kuunda ajira nzuri kwa kupunguza athari mbaya za mazingira na kukuza usalama na afya kazini unaosababisha biashara na uchumi endelevu wa mazingira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako